The House of Favourite Newspapers

MR BLUE ATAJA NCHI ALIOKIMBILIA

Image result for Khery Sameer ‘Mr Blue’

BAADA ya kutoonekana kwa muda hususan kwenye shoo ndani ya Bongo, rapa mkongwe kutoka kiwanda cha Muziki wa Bongo Fleva, Khery Sameer ‘Mr Blue’, ameibuka na kusema kuwa kwa sasa amejikita nchini Afrika Kusini ‘Kwa madiba’ na kwamba ameamua kufanya hivyo ili kubadili upepo.

Akichezesha taya na Star Showbiz, Mr Blue anayebamba na Ngoma ya Mbwa Koko alisema kuwa, kuwepo Kwa Madiba kumemfanya kujisikia tofauti na kuonesha hilo, juzikati alipafomu katika Jiji la Durban na kupata shangwe za kutosha kwa mashabiki wanaofutalia muziki wake.

“Nipo huku (Kwa Madiba) ikiwa ni muendelezo wa kazi zangu ambazo nimekuwa nikizifanya nje. Kwa sasa nimeamua kuwekeza nguvu zaidi kupiga dili za nje ya Bongo kama ambavyo nilikuwa nafanya ndani. Si vitu vigeni kwangu, lakini kwa sasa nahitaji kuipeleka kazi yangu next level zaidi.”

STAR SHOWBIZ

Comments are closed.