The House of Favourite Newspapers

Mr. Championi Agawa Zawadi Taifa kwa Wasomaji Wake

0

SAMSUNG CAMERA PICTURESMr.Championi akipozi na Msanii wa kuigiza kutoka kundi la Kashikashi la Mizengwe aitwaye, Jesca Kindole ‘Safina’ akipozi na Mr.Championi.

GAZETI Bora la Michezo hapa nchini la Championi kupitia kwa Mr.Championi leo liliingia mtaani na kugawa zawadi mbalimbali ikiwemo kuwarudishia fedha waliyonunulia wasomaji wake walokutwa wakilisoma ama  kununua gazeti hilo kwa wauzaji wa magazeti.

SAMSUNG CAMERA PICTURESWasomaji wa gazeti la Championi na gazeti pendwa la Risasi wakiyasoma magazeti hayo sambamba na Mr.Championi.

 

Baada ya kutua nje ya eneo la Uwanja wa Taifa wa Michezo jijini Dar es Salaam Mr.Championi kazi yake kubwa ilikuwa kuyanadi magazeti mawili ya Championi na Risasi Jumatanoambapo wasomaji mbalimbali walijipatia zawadi mbalimbali.

SAMSUNG CAMERA PICTURESWasomaji wakipozi na Mr.Championi.

Wasomaji hao walikuwa wakijiandaa na kufuatilia mechi ya Timmu ya Mpira ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting iliyokuwa ikichezwa jioni hii.SAMSUNG CAMERA PICTURES

Akizungumza na mashabiki wa mechi waliokuwa wamejitokezwa kwenye mtanange huoOfisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Yohana Mkanda, alisema anawaomba wasomaji wa magazeti hayo ya Global kuendela kulinunua Championi kwani  linakidhi kiu yao ya kupata habari za kimichezo.

SAMSUNG CAMERA PICTURESMr.Championi akimpatia zawadi msomaji wa Championi.

SAMSUNG CAMERA PICTURESMr.Championi akimpatia zawadi msomaji wa Championi.

 

Leave A Reply