The House of Favourite Newspapers

Mr. English Kuwanoa Kingereza Mastaa

0
James Mramba ‘Mr. English’.

JAMES Mramba ‘Mr. English’ aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa kuwafundisha watu mbalimbali lugha ya Kingereza, amewataka mastaa mbalimbali wafike kwenye darasa lake ili waweze kupata huduma yake.
Mr. English alisema kuwa, wasanii ni miongoni mwa watu ambao wanaitegemea lugha hiyo ili kufanya biashara yao katika nchi mbalimbali.

“Wasanii na watu wote wasisite kuja kwangu, ndani ya muda mfupi sana, ninawahakikishia watakuwa wamejua kuzungumza Kingereza,” alisema Mr. English.
Mr. English anatoa huduma hiyo katika ofisi yake iliyopo Sinza-Mapambano na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0713 369805 au 0767 369805 ili aweze kukuhudumia popote

Leave A Reply