The House of Favourite Newspapers

Mr Shinda Nyumba apagawisha Temeke leo

Mr Shinda Nyumba akigawa kuponi katika maeneo ya Temeke Stereo.

Shinda Nyumba akiwagawaia vipeperushi wakazi wa maeneo ya Temeke Stereo.

Mr Shinda nyumba akimsaidia kujaza kuponi ya Shinda Nyumba Geofrey John mkazi wa Chanika.

Ofisa usambazaji wa Global, Jimmy Harooub akiwapa maelekezo wakazi wa Temeke ya namna ya kujaza kuponi na kujishindia nyumba.

Jimmy akimsaidia Mohammed Hassan, mkazi wa Temeke kujaza kuponi.

Wakazi wa maeneo mbalimbali ya Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na Mr Shinda Nyumba.

Mr Shinda Nyumba akimjazia kuponi Aziz Ally, mkazi wa Temeke.

Jimmy akimjazia kuponi ya Shinda Nyumba Selemani Mohammed, mkazi wa Temeke.

Jimmy akimjazia kuponi ya Shinda Nyumba Mohammed Masiwa, mkazi wa Temeke.

Wasomaji wa magazeti ya Global wanaofanyia mishemishe zao maeneo ya Temeke Mti Pesa, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mr Shinda Nyumba (mwenye tisheti nyeupe na kepu nyukundu).

Godlisten Kisanga, mkazi wa Temeke akijaza kuponi ya Shinda Nyumba mbele ya Jimmy Haroub.

Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendelea hivi sasa chini ya Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa, Amani na Risasi inazidi kusonga mbele ambapo watu mbalimbali wanaendelea kujitokeza na kujaza kuponi kwa wingi ili kujitengenezea nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kila mwezi zikiwemo pikipiki na simu za kisasa  hatimaye kujishindia nyumba katika droo kubwa itakayochezeshwa hapo baadaye.

Huku bahati nasibu hiyo ikiendelea kuwa gumzo kutokana na msisimko iliyonayo wakati huu, leo yule Mr Shinda Nyumba anayesepa na kijiji kila kona anakopita, alikuwa mitaa ya Temeke na vitongoji vyake akizidi kuwapagawisha watu kutokana na urefu wake pamoja na namna ya kipekee anavyoitangaza promosheni ya Shinda Nyumba.

Mbali na kumshangaa Mr Shinda Nyumba na timu yake, wakazi wa maeneo hayo walijitokeza kwa wingi huku wakionesha dhahiri kupania kujishindia nyumba pamoja na zawadi mbalimbali kwa kununua magazeti kwa wingi pamoja na kujaza kuponi.

 PICHA: BONIPHACE NGUMIJE

 

 

Comments are closed.