The House of Favourite Newspapers

Mr Shinda Nyumba Azidi Kupagawisha Dar

Ofisa usambazaji Jimmy Haroub akiwa katika picha ya pamoja na wakazi mbalimbali wa Dar wanaofanyia mishemishe zao maeneo ya Kibaha.
Wasomaji wa magazeti ya Global Publishers wakazi wa Kibaha Dar wakimshuhudia mwenzao akijaza kuponi baada ya kununua gazeti.
Mr. Shinda Nyumba akimsaidia msomaji wa magazeti ya Global kujaza kuponi.
Mr. Shinda Nyumba akiwagawia wakazi wa Kibaha vipeperushi vya Shinda Nyumba.

Bahati na Sibu ya Shinda nyumba inayoendelea kwa sasa chini ya Kampuni la Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa, Amani na Risasi inazidi kusonga mbele ambapo watu mbalimbali wanaendelea kujitokeza na kujaza kuponi kwa wingi ili kutengeneza nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kila mwezi zikiwemo pikipiki na simu za kisasa hatimaye kujishindia nyumba katika druo kubwa itakayochezeshwa hapo baadaye.

Huku bahati na sibu hiyo ikiendelea kuwa gumzo kutokana na msisimko iliyonayo wakati huu, leo yule Mr Shinda Nyumba anayesepa na kijiji kila kona anakopita alikuwa mitaa ya Kibaha na vitongoji vyake akizidi kuwapagawisha watu kutokana na urefu wake pamoja na namna ya kipekee anavyoitangaza promosheni ya Shinda Nyumba.

Mbali na kumshangaa Mr Shinda Nyumba na timu yake wakazi wa maeneo hayo walijitokeza kwa wingi huku wakionyesha dhahiri kupania kujishindia nyumba pamoja na zawadi mbalimbali kwa kununua magazeti kwa wingi pamoja na kujaza kuponi.

Comments are closed.