The House of Favourite Newspapers

Ujenzi Wa Barabara Kidatu-Ifakara Wafikia Asilimia 82, RC Malima Atoa Maagizo Mazito

0
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima, akiangalia ujenzi unavyoendelea.

Morogoro 7 Novemba 2023: Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Mhe Adam Malima amemtaka mkandarasi anayesimamia mradi wa ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa kilomita 66.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami na daraja la Ruaha kufanya kazi usiku na mchana kuwezesha kukamilika kwa wakati.

Mafundi kazini.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kujionea hali halisi ya ujenzi wa barabara na daraja hilo, RC Malima amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua uchumi wa wananchi wa wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga

Mradi wa ujenzi wa barabara hiyo unafadhiriwa na mfuko wa maendeleo wa nchi za Ulaya (European Development Fund EDF) ukishirikiana na Shirika la Msaada wa Uingereza (UKAID) na Shirika la Kimarekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

RC Malima akimsikiliza kiumakini mkandarasi (aliyevaa kiakisi mwanga).

RC Malima amesema mradi huo utakapo kamilika unategemewa kuninua maisha ya mtu mmoja mmoja hasa wakulima wa Bonde la Mto Kilombero, uwekezaji uchimbaji madini Wilaya ya Ulanga.

Eneo la barabara inayokatisha kwenye daraja hilo.

Kwa upande wake, Mhandisi mkazi TANRODS Arnod Maeda amesema ujenzi mradi wote kwa ujumla barabara na daraja la Ruaha umefikia asilimia 82.8 na unatarajiwa kukamilika mwezi machi 2024 na unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi Bilion 128.    HABARI/PICHA ZOTE NA MWAJUMA RAMBO/ MOROGORO.

Leave A Reply