The House of Favourite Newspapers

Mrithi wa Zulu Yanga Ataka Gari, Nyumba

0
Mchezaji wa Yanga, Zulu

Wilbert Molandi | Championi Jumatano | Habari

KLABU kongwe ya Yanga imemweka kando kiungo wa Mbeya City, Kenny Ally kwenye mipango yake ya usajili katika msimu ujao huku chanzo kikiwa ni dau na mahitaji mengine binafsi. Kenny ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kwenye usajili wa msimu ujao wa Simba na Yanga kwa ajili ya kuviimarisha vikosi vyao.

Kiungo huyo, hivi karibuni kwenye mechi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu alionekana kuisumbua safu ya kiungo ya Simba iliyoongozwa na Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Said Ndemla huku akifanikiwa kufunga bao moja kwenye sare mabao 2-2.

Kiungo wa Mbeya City, Kenny Ally.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano kutoka kwenye Kamati ya Utendaji ya timu hiyo, kiungo huyo wameshindwana naye kutokana na mahitaji makubwa anayoyahitaji ili amwage wino wa kuichezea Yanga.

Mtoa taarifa huyo alisema, kiungo huyo anataka apewe dau la shilingi milioni 50, nyumba binafsi ya kuishi na gari atakalolitumia kwenye mizunguko yake ya kila siku.

“Kenny tulikuwa naye kwenye mazungumzo mazuri kwa ajili ya kumsajili katika msimu ujao wa ligi kuu, lakini mpango huo tumeachana nao kutokana na kushindwana kwenye maslahi. “Kikubwa kiungo huyo alikuwa akihitaji shilingi milioni 50 wakati sisi tukiwa na bajeti ya milioni 30 ambazo tulikuwa tayari kumpatia ili asaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga.

“Pia kiungo huyo aliomba apatiwe nyumba ya kuishi binafsi na gari la kutembelea la kwake yeye pekee ukiangalia vitu vyote hivyo ni gharama kubwa, hivyo tumeona tuachane naye na tutafute mchezaji mwingine mwenye sifa kama zake, kama baadaye atapunguza tutarudi kwake,”alisema mtoa taarifa huyo.

Kwa upande wake Kenny alisema “Sina sababu ya kutojiunga Yanga kama watanipatia mahitaji yangu ninayoyahitaji ikiwemo fedha shilingi milioni 50 na mahitaji mengine ninayoyahitaji, kumbuka soka ndiyo maisha yangu. Aidha kiungo huyo alisema, mkataba wake na Mbeya City unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo yupo tayari kujiunga na klabu yoyote itakayoonyesha nia ya kumsajili. Yanga imekuwa ikiwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara, lakini kwa msimu wa tatu sasa imekuwa na tatizo sana kwenye sehemu ya kiungo mkabaji ambayo kwa sasa anaichezea Justine Zulu ambaye bado hajaonyesha kiwango cha kuridhisha.

Leave A Reply