The House of Favourite Newspapers

Mrundi: Kwasi Hana Namba Simba SC

Asante Kwasi (kushoto).

BENCHI la ufundi la Simba chini ya kaimu kocha wake mkuu, Masoud Djuma raia wa Burundi limempa tahadhari beki mpya wa timu hiyo, Asante Kwasi raia wa Ghana kwamba anatakiwa kuendelea kuonyesha uwezo wa hali ya juu kwa ajili ya kuendelea kusalia katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

 

Kwasi alijiunga hivi karibuni na Simba katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa Desemba 15, mwaka jana akitokea Lipuli FC ya Iringa kwa dau la Sh milioni 25, ambapo tayari ameshatumika katika mechi tatu za timu hiyo katika Kombe la Mapinduzi kabla ya kutolewa na URA ya Uganda.

 

Mrundi huyo ameliambia Championi Jumatano, kuwa Mghana huyo asijiaminishe kwamba ana namba ya kudumu ndani ya kikosi hicho kutokana na yeye kubadili kikosi chake kutokana na mahitaji ya mechi husika lakini pia ushindani wa namba uliopo baina ya wachezaji wake.

 

“Ingawa kwa sasa tunamtumia zaidi Kwasi katika kikosi cha kwanza lakini siyo kwamba ndiyo ana namba ya kudumu katika timu hiyo, kwangu ninaangalia aina ya mechi na mahitaji ya watu ambao ninawataka hivyo ninaweza kupangua baadhi ya watu kutokana tu na aina ya mpinzani ambaye tunakabiliana naye.

 

“Lakini pia inabidi yeye aendelee kuonyesha kiwango kwani kama unavyojua hapa kuna wachezaji wengi wenye uwezo sasa ni lazima kwamba ili uendelee kudumu katika kikosi cha kwanza uonyeshe uwezo mkubwa zaidi ya wenzake, hawezi kuwa na uhakika wa namba kama hajitumi,” alisema Djuma. Simba ina mabeki sita wa kati ambao ni Kwasi, Juuko Murshid, Yusuph Mlipili, Salum Mbonde, Paul Bukaba na kiraka Erasto Nyoni.
Mrundi

Comments are closed.