Live: Msafara uliobeba mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa ukipita Arusha
Msafara uliobeba mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Lowassa ukipita katikati ya Jiji la Arusha leo Februari 15, 2024 kuelekea kijiji cha Ngarash, wilayani Monduli yatakapofanyika mazishi ya kiongozi huyo Jumamosi ya Februari 17, 2024 ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza mazishi hayo.