Msaidizi wa Membe Adaiwa Kutekwa

KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Allan Kiluvya ambaye anatajwa kuwa ni msaidizi wa Waziri mstaafu wa Mambo ya Nje ya wa Serikali ya awamu nne, anatajwa kupotea baada ya kuchukuliwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

 

Tukio hilo limetokea usiku wa jana alipokuwa na baadhi ya marafiki zake katika eneo la Mbezi jijini Dar es salaam.

 

Kwa mujibu wa mtu wake wa karibu ambaye amefahamika kwa jina moja tu la Magret, amesema mara ya mwisho yeye na Allan walikuwa pamoja wakitokea eneo la starehe, kabla ya kutokea kwa watu hao 7, wakiwa kwenye gari aina ya Land Cruiser ambayo ndiyo ilimchukua na kuondoka naye.

 

Aidha Magret ameeleza kuwa wameshatoa taarifa za awali kwa Jeshi la Polisi kwa ajili kuanza kwa uchunguzi wa kupatikana kwa Allan Kiluvya.

 

EATV/EARadio Digital imemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mussa Taibu kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo, ambapo amesema, “tumepata taarifa za tukio hilo kutoka kwa ndugu wa Allan, na sisi tunaendelea kulifuatilia kujua ni kwa namna gani alichukuliwa lakini siwezi kusema ametekwa kwa sababu bado hatujathibitisha”.

 

Juhudi za kumtafuta Bernard Membe bado zinaendelea.Msikilize Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinonfoni akizungumzia tukio hilo.

 

BABA DIAMOND ATINGA NA MKEWE KWENYE PARTY YA MAMA DANGOTE


Loading...

Toa comment