The House of Favourite Newspapers

MSAMA: SERIKALI IKO BEGA KWA BEGA NA WAFANYABIASHARA

0
Msama akizungumza na wanahabari.

 

MKURUGENZI wa Msama Promotions, wasimamizi na wasambazaji wa kazi za Muziki wa Injili, Alex Mwita Msama amesema serikali iko bega kwa bega na wafanyabiashara waaminifu wanaofuata utaratibu sahihi, ikiwemo ulipaji wa kodi kwa wakati na kuwataka watu wanaosambaza uongo wenye lengo la kuichonganisha na wafanyabiashara waache mara moja.

 

Katika mkutano wake na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar, Msama alisema serikali inashughulika na baadhi ya wafanyabiashara wanaokiuka misingi na taratibu za kibishara kama kukwepa kodi, hivyo wanapochukuliwa hatua stahiki hubaki wakisingizia mambo yenye kufitinisha, jambo ambalo si sawasawa.

 

 

Mazungumzo yakiendelea.

 

Pia, katika kuonesha msisitizo Msama alisema; “Serikali ya awamu ya tano ni serikali ya kazi, hivyo haina chuki na mfanyabiashara yeyote anayefuata utaratibu wa kawaida, ikiwemo kulipa kodi na mambo mengine ya kufanana na hayo.

 

“Lakini sasa niiombe serikali kama kweli inataka kukusanya kodi halali, basi ipige vita wachuuzi, wezi na maharamia wanaoiba kazi za sanaa kwa kuchoma CD feki, kwani kwa kufanya hivyo wananyonya jasho la wasanii na kuiingizia hasara serikali kwa kutolipa kodi halali, sisi kama wasimamizi na wasambazaji wa kazi za sanaa tumeazimia kufanya ufuatiliaji kwa oparesheni maalum, kuanzia Jumatatu wiki ijayo ili kuhakikisha tunapambana vya kutosha na tatizo hilo hivyo tunaiomba serikali ituunge mkono katika jambo hili.”

 

Leave A Reply