The House of Favourite Newspapers

MSANII MBARONI KWA KUTOA WIMBO WA KUMTUKANA RAIS

MAOFISA wa polisi wamemkamata mwanamuziki Moses Nsubuga maarufu kama Viboyo baada ya kutoa wimbo unaomkosoa Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni na spika wa bunge la nchi hiyo, Rebecca Kadaga.

 

Kwa mujibu wa msemaji wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa nchi hiyo, Vincent Ssekatte, Viboyo anashikiliwa katika Kituo cha Jinja Road kwa tuhuma za kutukana viongozi na kutoa kauli za kukebehi baadhi ya makabila nchini humo.

 

“Ndani ya wimbo wake, amewatukana viongozi wengi wa nchi na wa makabila ya Uganda, jambo ambalo ni kosa kisheria. Amekuwa akijificha kwa siku nyingi wakati tukimsaka lakini bahati nzuri tumemkamata jijini Kampala na tunaendelea kumshikilia kwa mahojiano,” alisema Ssekatte jana.

 

Polisi wamedai ndani ya wimbo huo, Viboyo ametumia lugha ya Kabila la Luganda kuwatukana viongozi akisema amechoshwa na uongozi wa Taifa la Rwanda lakini pia akimtukana matusi ya nguoni Rais Museveni, jambo ambalo ni kosa kubwa. Pia amewashutumu viongozi wa nchi hiyo kwa mauaji ya aliyekuwa Msemaji wa Jeshi la Polisi, Andrew Felix Kaweesi na Andrew Kayiira ambapo leo Ijumaa atatakiwa kutoa maelezo.

 

Kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Uganda, mtu yeyote anayetumia mawasiliano ya kielektroniki kujaribu kuvuruga au kuharibu amani ya nchi, amefanya kosa na anaweza kuhukumiwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja jela, kulipa faini ya Sh 480,000 za Uganda au vyote kwa pamoja.

 

Source: Daily Monitor

Comments are closed.