Msanii Tekno Miles kunogesha tamasha la Johnnie Walker
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini mkutano wa kumtambulisha Msanii maarufu Tekno Miles kutoka Nigeria uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambaye anatarajiwa kutumbuiza katika mkesha wa Tamasha la Grown and Sexy the Gold finale litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite jijini Dar es salaam.
Maandalizi ya Tamasha maarufu la Johnnie Walker “Grown and Sexy The Gold finale” kwa ajili ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya yanaendelea vizuri ambapo kwa mujibu wa waandaaji wa Tamasha hilo, “Capital events” kupitia wadhamini wao “Johnnie Walker” chapa maarufu ya pombe kali inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti wamemleta Msanii Tekno Miles kutoka Nigeria kutumbuiza laivu katika Tamasha hilo ambalo litakua la mwisho kabisa katika historia ya matamasha ya Grown and Sexy nchini Tanzania.