The House of Favourite Newspapers

Msanii wa Bongo Fleva Lulu Diva Adaiwa Kulazwa Hospitali

0

LULU Abbas almaarufu Lulu Diva; ni mrembo mkali kunako Bongo Fleva na Bongo Movies ambaye anadaiwa kulazwa hospitalini kwa mshtuko baada ya video yake chafu kuvuja na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

 

Jana Alhamisi, Gazeti la IJUMAA lilifika nyumbani kwake maeneo ya Mbezi[1]Beach jijini Dar ambapo hakuwepo nyumbani, lakini kwa mujibu wa majirani, walisikia Lulu Diva amelazwa hospitalini.

 

Hata hivyo, koneksheni ya Lulu Diva imewaibua watu weni ambao wanasema kuwa ishu hiyo iwe funzo kwa kina dada ambao wamekuwa vichwa ngumu kujifunza kwa wenzeo.

 

Imeelezwa kuwa, mara zote ambazo video hizo zimesambaa, basi asilimia 90 ya video hizo anayeonekana kuathirika, kushambuliwa mwanamke. Kifupi imeelezwa kuwa, koneksheni ya mwanaume inakuwa kama siyo ishu kubwa na watu hawajali kivile, lakini zinapovuja za kina dada inakuwa ni ishu kubwa.

Wataalam wanasema kuwa, mtu anayetaka umtumie picha au videos zako za utupu ni kuwa hana malengo na wewe na wala hakuheshimu ila anayekuheshimu siyo rahisi kukurekodi au kukuambia jirekodi umtumie hivyo cha muhimu ni kumkimbia au kumkataa mtu au mpenzi anayehitaji mambo kama hayo.

Leave A Reply