The House of Favourite Newspapers

Msanii wa Gospel, Noella Alain Atoa Ushauri kwa Wasanii wa Muziki wa Injili

0

Msanii wa muziki wa Gospel, Noella Alain @noelamartha anayefanya vizuri na wimbo wa Roho ya Mazoea, amesema kuimba muziki wa injili ni jambo linalotakiwa kutoka ndani ya moyo wako kwa lengo la kutoa huduma kwa njia hiyo lakini kama ukiimba kwa lengo la kupata fedha kamwe huwezi kufanikiwa.

Ameyasema hayo leo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha #DsmFlavour na kueleza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo kwa miaka mingi lakini hachoki kwa sababu ni jambo analolipenda kutoka ndani ya moyo wake.

Miongoni mwa kazi nyingine zilizompa umaarufu Noella ni pamoja na wimbo wa Mwamba aliomshirikisha Bonny Mwaitege, Mungu Yupo aliomshirikisha Ambwene Mwasongwe na nyingine nyingi.

 

Leave A Reply