Msanii wa Harmonize Awashukuru Mashabiki Kwa Kumpokea

Msanii kutoka katika lebo ya Konde Music Word Wide, Ibraah.

MSANII kutoka katika lebo ya Konde Music Word Wide Ibraah,  leo Mei 21, 2020 amefanya mahojiano katika kipindi cha Bongo 255, kinachorushwa Jumatatu hadi Ijumaa saa sita hadi saa 10 jioni, kupitia spika za +255 Global Radio, zilizopo Sinza Mori jijini Dar kinachosimamiwa na Stewart George na Lady T.

 

Ibraah alikuja katika studio hizo, kutambulisha wimbo wake wa One Night Stand aliomshrikisha Harmonize, pamoja na kuitangaza Extend Play (EP), ambayo pia inafanya vizuri sokoni kwa sasa.

Wakati akitambulisha kazi hizo, Ibraah alimpongeza Harmonize kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuonyesha kipaji chake kwa watanzania, lakini pia aliushukuru uongozi wa Konde Music World Wide kwa kufanikisha kila kitu hadi sasa watanzania wanamsikia na kumfahamu.

Pia amewashukuru mashabiki kwa kupokea kazi zake na kumfanya kuwa moja ya wasanii wanaosikilizwa sana kwa sasa nchini, huku akiongeza kuwa bila wao yeye hawezi kuwa na nguvu ya kujituma kufanya kazi kwa juhudi na maarifa. Ambapo alitumia nafasi hiyo kuiipongeza Global Publishers kwa kumtangaza kwenye magazeti, Tv na radio.

“Nimshukuru sana kaka yangu Harmonize kwa kuweza kuniamini na kunipokea kwa moyo wote na kunipa nafasi ya kuweza kuufanya mziki wangu, lakini pia nitumie nafasi hii kuwashukuru viongozi wote wa Konde Music World Wide ambao wamekuwa wakifanya juhudi kubwa kutoka siku ya kwanza wananipokea na kufika hapa nilipo leo.

 

“Lakini mashabiki nao niwashukuru, maana wameweza kunipokea vizuri sana na kazi zangu sasa zinachezwa sehemu nyingi, sisi wasanii huwa tunafanya kazi kwa ajili yao, kwahiyo bila wao mimi siwezi kuwa na moyo na juhudi ya kufanya kazi kwa bidii, Mungu awabariki sana,” alisema Ibraah.

 

“Baada ya Steps, kitachofuata ni album, kwa sasa nakesha sana studio nikirekodi nyimboa lisema, Harmonize ameshamaliza kazi yake, kilichobaki ni mimi kutumia akili yangu ili niweze kufika mbali zaidi ya hapa nilipo kwa sasa.

“Naweza nikafanya kazi kwenye lebo yoyote hata kama WCB wakiona nafaa, lakini hiyo itakuja kutokea kama uongozi wangu wa sasa utaachana na mimi, kwa sababu mziki ndiyo kazi yangu na nitafanya popote, kikubwa ni maslahi tu,”

“Sina elimu ya kujitosheleza, itabidi nisome ili niwe wa kimataifa zaidi,”

“Wandoto ni ngoma ambayo mimi naipenda zaidi, nimeimba kwa hisia sana, japo zipo ngoma nyingi watu wanazipenda,”

“Wote sisi ni watanzani, naweza nikajiunga WCB kama nikitoka Konde Music wameniacha,”

“Nasikiliza mziki wa Zuchu, ni msanii mzuri na nipo tayari kufanya naye kazi,”

“Nisipofanya kazi nzuri naweza kuondoka Konde Music, kwa sababu nitakuwa siingizi faida na uongozi unaweza ukanitema,”.

“Nilishapita kwenye studio nyingi na kukutana na wasanii wengi lakini hakuna aliyewahi kunipa msaada au kunisiaidia,”

“Sijawahi kuumizwa kwenye mapenzi ila nilishawahi kuenjoy mapenzi,”

“Nilikuwa na mpenzi ila tuliachana muda mrefu sana na hatukudumu. Hanitafuti kwa sababu yeye ndiye alinikataa,”

“Nipo Singo, naweza kuwa na mwanamke yeyote ambaye tutaelewana na kuelewa kazi ninayofanya,”

“Sikupenda Hamornize aingie kwenye wimbo wangu wa One Night, lakini yeye aliupenda akaomba kuingiza Vesi,”

“Wale wanawake wa kwenye video ya One Night walinipa changamoto sana wakati wa kurekodi, si unajua ambavyo walivyo warembo,”

“Nasikiliza wasanii wengi sana, tofauti tofauti wa Tanzania, lakini siwezi kuwataja majina wote,”

“Nashukuru kupata nafasi ya kuja hapa, kwa sababu hii ni sehemu ambayo kila msanii anatamani kuja, kwa sababu nyinyi mnafanya tuwafikie hadi wale ambao hawapo Instagram,” alisema Ibraah msanii wa Konde Music.


Loading...

Toa comment