The House of Favourite Newspapers

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI ATINGA MAONYESHO YA SADC

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, akisoma kipeperushi cha bidhaa inayozalishwa na kampuni ya ushonaji ya Malika Designer alipotembelea banda hilo katika Maonyesho ya Wiki ya Viwanda ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Viwanja vya Karimjee na Gymkana Jjjini Dar es Salaam.  Kulia kwake ni mmiliki wa kampuni hiyo, Malika Rashidi.

MSEMAJI  Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi, Agosti 7, 2019 ametembelea Maonyesho ya Wiki ya Viwanda kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Viwanja wa Karimjee na Gymkana jijini Dar es Salaam.

…Akiwa na wafanyakazi wa Wakala wa Vipimo, Ukaguzi wa Bidhaa Zilizofungashwa alipotembelea banda lhilo.
…Akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Ukanda wa Uzalishaji wa Mauzo ya Nje (EPZA), George Karumuna na Zubeda Elias.
…Akiangalia moja ya bidhaa za korosho zinazozalishwa na Kampuni ya Tan Korosho. alipotembelea banda la  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).  Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa (TanTrade), Edwin Rutegaruka.
…Akipata maelezo kutoka kwa Ben Mwanantala wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kuhusu ujenzi na ufanyaji kazi wa reli ya kisasa (SGR).
…Akifafanua jambo mbele ya wafanyakazi wa Kampuni ya Tanzanitie Founder Foundation, kuhusu kuyatangaza madini ya Tanzanite.
…Akipokea kitabu kinachohusu utafiti na Uchenjuaji Madini kutoka kwa Mhandisi Mchenjuaji Madini Mwandamizi, Priscus Kaspana.

Comments are closed.