The House of Favourite Newspapers

Msemaji Mkuu wa Serikali Azungumza na Wanahabari Dodoma (Picha+Video)

0
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya Serikali katika mkutano na waandishi wa habari leo Juni 12, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi za Idara ya Habari-MAELEZO, Dodoma.

 

“Ujenzi wa awamu ya kwanza wa majengo ya Serikali katika mji wa Serikali Mtumba umekamilika kwa 100% kwa gharama ya Shilingi bil. 39, hivi sasa tunatekeleza awamu ya pili ambapo tutatumia Shilingi bil. 621 hadi tutakapokamilisha ifikapo Oktoba, 2023”

 

“TFS na TARURA wanapanda miti 500,000 katika Mji wa Serikali ili kuweka mandhari nzuri ya Ofisi za Umma. Eneo hili la Mji wa Serikali limejengwa barabara nzuri za lami zenye urefu wa kilometa 51.2 na kazi imefikia 99% ”

 

“Kwa Mwaka huu wa Fedha,Serikali imeidhinisha bil. 372.6 kwa ajili ya Jiji la Dodoma ambapo Sh.bil.72 zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ya mzunguko,Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato,eneo la wafanyabiashara wadogo na miradi ya maji”

“Tutakuwa na Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ambapo kwa sasa maandalizi yamefikia asilimia 88. Mwaka huu tutakuwa na madodoso yafuatayo; Dodoso la msingi la Sensa, Dodoso la makundi maalum, Dodoso la jamii, Dodoso Majengo na Dodoso la Anwani za Makazi”

 

“Nawaomba wananchi kuichukulia jambo la Sensa kuwa la kitaifa kwa umuhimu wa kipekee, tunataka tuandike historia ya kuwa nchi iliyofanya Sensa kwa viwango vya ubora wa hali ya juu”

 

“Tunawapongeza ambao wameweka vibao vya nyumba zao, na Serikali inatoa wito kwa Watanzania wote kuweka vibao vya nyumba zao baada ya kuwa wamepatiwa anwani. Nguzo za majina ya mitaa zinawekwa na TARURA kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa” amesema Gerson Msigwa

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply