The House of Favourite Newspapers

Msemaji wa Serikali: Tanzania Kutapata Chanjo Milioni 11 – Video

0

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Agosti 1, 2021 akizungumza na Watanzania katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu Utekelezaji wa Serikali katika Sekta Mbalimbali, Mkutano huo unafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

 

”Rais Samia Suluhu anafanya kazi kubwa sana kuhakikisha Tanzania inapata chanjo nyingi iwezekanavyo, kwasababu nchi yetu imejiwekea tupate asilimia kama 60 hivi ambapo tutakuwa tumejihakikishia kukata maambuzi ya ugonjwa huu wa Uviko-19”

 

”Nchi zote zitasaidiwa chanjo kwa idadi ya asilimia 20 ya watu wake, kwahiyo Tanzania kupitia mpango huu tutapata takribani chanjo milioni 11, kwahiyo zilizokuja hizi zaidi ya milioni 1 ni sehemu ya mpango wa COVAX Facility chini ya WHO”

”Zoezi la chanjo litaanza kutolewa kesho kuna vituo kama 550 vilivyoandaliwa, chanjo hazijaleta madhara kwa waliotumia kama tulivyokuwa tunasikia. Chanjo zitaendelea kuletwa baada ya zile dozi milioni 1 kuna nyingine zitaendelea kuletwa”

”Tungependa wananchi kwenye suala hili la chanjo wajitajidi sana kuwasikiliza wataalam wetu wanasemaje, maana hivi sasa kila mtu amejivisha utaalam anaijua Corona lakini serikali imetoa muongozo na ni vyema watu wausome na kuufuata”

 

“Msimamo wa Serikali ni kwamba shughuli ziendelee kama kawaida lakini Watu wachukue tahadhari, Wizara ya Afya imeandaa Mdahalo kesho pale Muhimbili wale wote wenye hoja waende wakatoe hoja zao watajibiwa, hoja inajibiwa kwa hoja”

 

“Serikali imetekeleza ahadi ya kulipa madiwani wa halmashauri ambazo mapato yake si makubwa na hazipo daraja A, mishahara yao inalipwa moja kwa moja kutoka Hazina na tayari madiwani wanalipwa Sh. laki tatu na wenyekiti wao Sh. laki nne”

 

”Wafanyakazi wote wa serikali wanalipwa mishahara kabla ya tarehe 25 ya kila mwezi hivi navyozungumza tayari mishahara wa mwezi Julai wameshalipwa. Jumla ya Bilioni 630 zimelipwa tarehe 23” amesema Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa

Leave A Reply