Mshambuliaji Neymar Jr Ajiunga na Miamba ya Saudi Arabia, Al Hilal
Mshambuliaji, Neymar Jr amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na miamba ya Saudi Arabia, Al Hilal kwa ada ya uhamisho ya euro milioni 90 kutoka Paris Saint-German.
Neymar (31) raia wa Brazil amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo mpaka Juni 2025 na atalipwa mshahara wa Euro milioni 150 (≈ Tsh bilioni 410).