The House of Favourite Newspapers

Mshindi Wa App Ya Global Radio Apatikana, Apewa Ofa Ya Chakula

Mshindi wa kwanza wa shindano la kupakua App ya +255 Global Radio, Iddy Sudi akipata chakula katika Hotel ya The Atriums iliyopo Afrikasana, Sinza, Dar es Salaam.

MSHINDI wa kwanza wa shindano la kupakua App ya +255 Global Radio, Iddy Sudi  leo Alhamisi Oktoba 3, 2019 amefika Hotel ya The Atriums iliyopo Afrikasana, Sinza Dar es Salaam kupata chakula cha mchana akiwa ameongozana na mtangazaji wa Kipindi cha Katambuga kinachoruka kupitia +255 Global Radio,  Aisha Hussein ‘Odo Aisha’.

 

Akiongea na mtandao huu, Iddy amesema mara yake ya kwanza aliona post kwenye ukurasa wa Instagram wa Global Publishers ukitangaza kupakua App kusikiliza na kushinda ndipo alipohamasika na kuamua kuwa mwanafamilia wa kudumu.

 

“Haikuwa kushinda tu bali kubadili mazingira na aina ya watu nitakaokutana nao,” alisema Iddy Sudi, mshindi wa +255 Global Radio aliyepakua App na kushiriki katika mijadala mbalimbali inayoendelea katika vipindi vya Radio hiyo mara baada ya kuwasili katika ya The Atriums.

Pamoja na yote ameahidi kuwa balozi mzuri wa kuitangaza vyema +255 Global Radio huku akiwataka watu washtuke maana mamilioni ya watu wanamiliki radio kwenye viganja vyao.

 

Shindano hilo bado linaendelea, unachotakiwa kufanya ni ku-install App ya Global Radio kutoka Google Play Store au App Store baada ya hapo una-screenshot muonekano wa App na kutuma kwenda kwenye WhatsApp ya Global Radio; +255 746244255 utajishindia vocha na zawadi ya kupata chakula cha mchana au ofa ya kulala katika Hoteli ya The Atriums.

Mbali na zawadi hizo, zipo nyingine kemkem, shiriki na ushinde!

Comments are closed.