R Kelly Anyimwa Dhamana Arudishwa Rumande

MWANAMUZIKI mkongwe wa miondoko ya Pop Bwana Robert Kelly “RKelly” baada ya kukaa rumande kwa wiki kadhaa sasa amenyimwa  dhamana kwenye shtaka lake la Unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo, Ataendelea kukaa ndani hadi kesi itakapoanza kusikilizwa tena.

Jana Jumatano mwana sheria wa R Kelly, Kellz alifikisha  maombi  ya dhamana Mahakamani mjini New York amedai kuwa mteja wake amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya tangu alivyoingia Jela, Hata hivyo Jaji wa mahakama hiyo Ann Donnelly ametupilia mbali ombi hilo na kusema kufanya hivyo kuna hatarisha usalama wa mashahidi na pia huwenda akatoroka.

R Kelly ataendelea kubaki Jela hadi Mei 18, 2020 ambapo Shauri lake limetajwa kusikilizwa tena.

Toa comment