The House of Favourite Newspapers

Mshindi wa Milioni 188.5 za M-BET kuichangia Yanga

Mshindi wa droo ya kwanza  ya mwaka huu ya Perfect 12 ya kampuni ya M-BET Frank Kayombo (wa pili kushoto) kutoka mkoa wa Njombe  akipokea mfano wa hundi ya Sh milioni 188.5 kutoka kwa meneja Masoko wa M-BET, Allen Mushi (wa pili kulia). Wengine katika picha ni Afisa wa Michezo ya Bodi ya Kubahatisha Catherine Lamwai (wa kwanza kulia) na Philipo Haule afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)Wilaya ya Ilala jijini Dar.

 

Dar es Salaam. Mkazi wa Njombe, Frank Kayombo (24) ameshinda Sh.188,484,550 kwa kubashiri kiusahihi Mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet.

 

 

Kayombo ambaye  shabiki wa timu za Yanga na Manchester United ya Uingereza  amekuwa mshindi wa kwanza wa droo ya M-BET kwa mwaka huu.

 

Meneja Masoko wa Kampuni ya M-BET Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa  M-Bet inaendelea kuwa nyumba ya mabingwa kwa kubadilisha maisha mbalimbali ya watanzania.

 

 

Mushi alisema kuwa serikali imejipatia Sh38 millioni ikiwa ni kodi ya ushindi asilimia 20 na  kuchangia pato la taifa.

 

 Alisema kuwa droo yao ya Perfect 12 inazidi kutoa washindi na kuchangia maisha kwa Watanzania ambao wamekuwa wakijishindia mamilioni ya fedha kila wakati.

 

 

“Huu ni mwanzo wa mwaka na tayari M-BET imetoa mshindi wa mamilioni ya fedha ambaye ataweza kujiendeleza kimaisha  na vile vile kuchangia taifa lake. M-Bet tunajivunia kuwa kampuni pekee ambayo mpaka sasa imewafaidisha watu wengi kupitia michezo yake, naomba Watanzania kuendelea kubashiri na kampuni michezo yetu kwa njia ya mitandao, simu ya mkononi na mengineyo,” alisema Mushi.

 

 

Kwa upande wake, Kayombo alisema kuwa alitumia Sh 1,000 na kubahatika kushinda droo hiyo ya kwanza ambapo atatumia fedha hizo kwa ajili ya kujiendeleza, kufungua miradi na vile vile kununua nyumba.

 

Kayombo ambaye ni mfanyabiashara ya miamala ya fedha kwa njia ya simu, alisema kuwa ndoto yake kubwa ni kupata maendeleo makubwa katika biashara zake na kuweza kuisaidia familia yake.

 

 

“Nina furaha sana kupata kiasi hiki cha fedha ambacho kwa kweli ni kikubwa ukilinganisha na kiasi nilichotumia kubashiri, Naona mwanga wa maisha yangu na familia kwa ujumla. Naishukuru M-BET kwa kuonyesha uaminifu kwangu na kwa washindi wengine,” alisema Kayombo.

 

 

Mshindi huyo pia alisema atatumia kiasi cha fedha alizoshinda kuichangia timu yake ya Yanga kupitia namba maalum iliyotangazwa kwenye vyombo vya habari. “Naipenda Yanga na kiasi ambacho nitawapa timu yangu kinabakia kuwa siri,” alisema.

 

Kaimu Msimamizi wa Kitengo cha Michezo ya Kubahatisha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Philipo Haule aliipongeza M-BET kwa kuendelea kuchangia pato la Taifa.

Comments are closed.