The House of Favourite Newspapers

Mshtuko Ray C kutaka kujiua!

 

DAR ES SALAAM: Mshtuko! Sexy lady kutoka Bongo Flevani, Rehema Yusuf Chalamila ‘Ray C’ ameibua mshtuko mkubwa kwa mara nyingine baada ya kudai kuwa anajihisi mnyonge na anaonelea ni vema ajitoe uhai ili akapumzike.

 

Mapema wiki hii, Ray C kupitia jumbe kadhaa za kutatanisha alizozichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, alisema ana mawazo mengi ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda.

 

“Mwaka huu nahisi kama nitajiua, nina mawazo mengi sana,” aliandika Ray C kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram.

Kwa upesi wafuasi wake, waliingilia kati na kutaka kujua kulikoni huku wakimtaka kutafuta ushauri badala ya kuchukua hatua hiyo.

 

Hata hivyo, wengine walidai, Ray C ana mazoea ya kutishia kujitoa kujiua mara kwa mara, mbinu waliyodai yeye hutumia kujitafutia umaarufu baada ya kudidimia kimuziki.

 

Ray C aliwahi kupelekwa katika kituo cha kurekebishia tabia (sober house) baada ya kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya. Ray C kwa sasa ana makazi nchini Uingereza baada ya kupata mchumba mtasha huku akiendelea kupiga shoo kwenye nchi mbalimbali barani Ulaya.  

Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA

Comments are closed.