The House of Favourite Newspapers

Msuva Atua Bongo Kupumzika, Apokelewa Kwa Mahojiano (Video)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco, Simon Msuva, akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Dar leo.
…Akisalimiana na wanahabari.
…Akifanya mahojiano na Global TV Online na mwandishi wa Gazeti la Championi, Wilbert Molandi (kushoto).

MSHAMBULIAJI  wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika club ya Difaa El Jadid ya Morocco, Simon Msuva, leo asubuhi amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, akitokea Morocco kwa ajili ya mapumziko mafupi baada ya ligi nchini humo kusimama.

 

Msuva ameichezea timu yake ya Difaa El Jadid michezo 14 ya raundi ya kwanza kati ya 15 ya Ligi Kuu. Global TV Online ilikuwepo wakati wa mapokezi ya mchezaji huyo.

(PICHA: MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS)

Comments are closed.