The House of Favourite Newspapers

MTAA KWA MTAA: MZEE ALIYEPEWA BARABARA NA JPM -VIDEO


WIKI kadhaa zilizopita, mzee Rashid Mashawishi alisimama mbele ya Rais Magufuli na kumweleza kero zilizopo mtaani kwake akiwa mwenyekiti ambapo alisema moja ya kero hizo ni ubovu wa miundombinu ya barabara ambapo katika kumjibu, Magufuli  alitoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda , kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa na barabara ikishajengwa iitwe jina la Rashid Mashawishi.

Magufuli alikuwa ametembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa msikiti wa Mtambani, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, ambao unajengwa  kwa ufadhili wa Mfalme wa Sita wa Morocco.

 

Global Tv imefunga safari mpaka kwa mwenyekiti huyo wa Mtaa wa Kinondoni-Shamba na kuzungumza naye kuhusu ujenzi wa barabara hiyo na vitu vingine kuhusiana na mtaa wake.

Comments are closed.