Mtanzania Atunukiwa na Umoja wa Mataifa kwa Kutengeneza Chujio

MHANDISI mmoja nchini Tanzania, Dkt. Askwar Hilonga, ametambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa uvumbuzi wake wa kifaa cha kuchuja maji chenye gharama ya chini ambacho kinalenga kubadilisha maisha ya wakazi wasio na maji safi ya kunywa.

 

Dkt. Hilonga ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia,  alitunukiwa tuzo hiyo wakati wa mkutano wa WHO mjini Geneva, Switzerland. Alikuwa akihudhuria mkutano wa bodi ya Afya Duniani, inayotoa maamuzi ya WHO.

 

Bodi hiyo huwakilishwa na wajumbe kutoka mataifa wanachama wa WHO na huangazia ajenda maalum zilizoandaliwa na bodi kuu. Akisukumwa na ari ya kukabiliana na magonjwa yanayoambukiza kupitia maji , Hilonga alisomea shahada ya uzamivu ya Nano-technolojia ambayo inashirikisha utumiaji wa atoms na molecules kwa utengenezaji wa bidhaa.

 

Dkt. Hilonga alivumbua kichujio hicho cha maji cha gharama ya chini kinachotokana na teknolojia hiyo ya nano, na tangu wakati huo amepata tuzo katika mashindano tofauti ya kisayansi ambayo yametunza umaarufu wake mbali na kumkabidhi fedha kufadhili kampuni yake ya Gongali Model Company.

 

Chujio hicho cha cha maji kinachotumia mchanga kusafisha maji ya kunywa kwa kutumia mfumo wa nano-teknolojia, tayari kina nembo yake.

 

“Ninaweka maji kupitia mchanga ili kuzuia uchafu na bakteria, lakini mchanga hauwezi kuondoa uchafu kama vile fluoride na madini mengine mazito hivyo nitapitisha kupitia vifaa vya nano ili kuondoa kemikali,” alisema Mr Hilonga.

Anasema kwamba awali chujio moja lilikuwa likigharimu $130, lakini akasema kuwa atanunua vifaa na kupunguza bei baada ya kushinda £25,000 .

“Kwa watu ambao hawawezi kununua chujio la maji, tumeanzisha vituo vya maji ambapo watu watakuja kununua kwa bei nafuu”, aliongezea.

 

Katika kanda yake ya video katika mtandao wa Youtube,  Hilonga anelezea kwamba chujio hilo linaweza kuondoa uchafu kwa hadi asilimia 97, lakini lengo lake kuu lilikuwa kutengeza chujio ambalo linaweza kuzuia asilimia 99.9 ya bakteria pamoja na virusi.

 

Familia yake ilikuwa ikikumbwa na magonjwa yanayoasababishwa na maji nchini Tanzania, hivyo alipofuzu shahada yake ya uzamivu katika nanoteknolojia nchini Korea Kusini alianza kukusanya vifaa vya nano ambavyo vitasaidia kusafisha maji.

 

Taasisi ya wahandisi ya Royal Academy inalenga kuwasaidia wahandisi waliopo katika jangwa la Sahara kutafuta suluhu za changamoto zinazokokumba Afrika kuwa biashara.

Hilonga na wahandisi wengine watatu , walipokea £10,000 kila moja ili kuanzisha mradi wa kibiashara.


Loading...

Toa comment