The House of Favourite Newspapers

Mtanzania Auawa Afrika Kusini

RAIA wa Tanzania aliyekuwa mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Johannesburg (UJ) nchini Afrika Kusini, Baraka Nafari ameuawa baada ya kugongwa na gari na watu wasiojulikana akitokea katika matembezi ya usiku.

 

Akizungumzia suala hilo, Waziri  wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga amesema bado ofisi yake haijapata taarifa yoyote rasmi kuhusiana na kifo hicho. Licha ya kuwa nje ya ofisi, amesema hadi asubuhi hakukuwa na taarifa kutoka Ubalozi wa Afrika Kusini kuhusu kijana wa Kitanzania kufariki nchini humo.

 

“Ngoja niwasiliane na wenzangu waliopo ofisini na ubalozi wetu nchini Afrika Kusini kwa maelezo zaidi, kama limetokea wakusanye taarifa za kina kabla ya kuzituma, hilo linaweza kuchelewesha kutufikishia taarifa mapema,” amesema Balozi Mahiga.

Mtanzania Auawa Afrika Kusini

Comments are closed.