The House of Favourite Newspapers

Yanga Wapelekwa kwa Babu Singida, Kazi Ipo!

Droo ya upangaji wa timu zitakazokuwa zinacheza hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho imefanyika asubuhi ya leo katika makao makuu ya Azam TV yaliyopo Tabata, Dar es Salaam.

Upangaji huo ulihusisha timu nane ambazo ziliingia hatua ya robo fainali ya mashindano hayo, timu hizo ni Yanga, Stand United, Azam FC, JKT Tanzania, Mtibwa Sugar, Singida United, Njombe Mji na  Tanzania Prisons ambapo Yanga watakutana na kocha wao wa zamani, Hans van Pluijm (Babu) anayeinoa Singida Utd.

Baada ya droo kupangwa, timu zitakozokutana katika hatua hii ni hizi

Singida United v Yanga
Tanzania Prisons v JKT Tanzania
Azam FC v Mtibwa Sugar
Stand United v Njombe Mji.

Comments are closed.