The House of Favourite Newspapers

Mtanzania Elizabeth Mrema Ateuliwa Kuongoza Shirika la Umoja wa Mataifa

0
Elizabeth Maruma Mrema kutoka Tanzania.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Elizabeth Maruma Mrema kutoka Tanzania kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira (UNEP).

Bi. Mrema atamrithi Joyce Msuya kutoka Tanzania aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa Masuala ya Kibinadamu na Naibu Mratibu wa Misaada ya Dharura katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA).

Elizabeth amehudumu katika nafasi mbalimbali ambapo tangu mwaka 2020 amehudumu kama Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Bayoanuai (CBD), yenye makao yake mjini Montreal, Canada.

Hapo awali aliwahi kuwaKaimu Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya CBD na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika shirika la UNEP huko Nairobi, Kenya, pamoja na kuwa Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Mkataba wa Sekretarieti ya Wanyama Wanaohama yenye makao yake makuu mjini Bonn, Ujerumani.

LOWASSA BADO AMELAZWA AFRIKA KUSINI, WAZIRI MKUU AMJULIA HALI HOSPITALINI AKIMWAKILISHA RAIS SAMIA..

Leave A Reply