The House of Favourite Newspapers

Mtendaji Mkuu wa Man United Ed Woodward Ajiuzulu

0

MTENDAJI mkuu wa klabu ya Manchester United ya England, Ed Woodward amejiuzulu wadhifa huo baada ya kuwa mmoja wa viongozi waliohusika  kwenye wazo  la  kuanzishwa wa European Super League.

 

Hatua ya kujiuzulu  imekuja baada ya shinikizo kubwa kutoka  mashabiki wa vilabu sita ambavyo ni Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham, kuandamana  wakishinikiza vilabu hivyo kutoshiriki kwenye michuano hiyo.

 

Jana Aprili 20 mchezo kati Chelsea dhidi ya Brighton ambao uliisha kwa sare tasa (0-0) ulilazamika kuchelewa kuanza kwa takriban dakika 40, baada ya mashabiki kufurika nje wa uwanja w Stamford Brigde, wakishinikiza Klabu hiyo kuachana na mpango huo.

 

Mpango huo ulionekana una lengo la kuzinufaisha timu hizo kubwa na kuweka rehani uhai wa timu ndogo na zakati ambazo hazina fedha nyingi.

 

Awali Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (Uefa) ilitoa onyo kali kwa wachezaji ambao wangeshiriki ligi hivyo wasingepata vibali vya kucheza kwenye timu zao za taifa kwenye michuano ambayo inasimamiwa na shirikisho hilo.

 

Ed Woodward ambaye alijiunga na United  mwaka 2005, amedumu katika wadhifa huo kwa miaka 8 tangu 2013-2021, ataachia ngazi mwishoni mwa msimu huu.

 

Leave A Reply