The House of Favourite Newspapers

Mtihani No. 1 kwa wakuu wapya wa mikoa tz

1

pombe2Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’.

Oscar Ndauka, AMANI

DAR ES SALAAM! Tayari Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ ameshawaapisha wakuu 26 wa mikoa yote ya Tanzania Bara, lakini kubwa ambalo ndiyo mtihani kwao ni kauli ya rais kwamba, wakapambane kuwaondoa watumishi hewa ambao wanalipwa mishahara wakati hawapo.

Kauli hiyo ya JPM imechukuliwa na wadau kama ndiyo changamoto kubwa katika halmashauri nyingi nchini ambapo katika marais wote waliomtangulia, wamekumbana na watumishi hewa kulipwa mishahara.

“Magufuli kawaambia wakuu wapya wa mikoa wakahakikishe mikoa yao haina njaa, pia amewaagiza kuhakikisha wanawasimamia watu kufanya kazi lakini mimi nasema hiyo siyo mitihani mikubwa. Suala la kuwepo kwa watumishi hewa ndiyo mtihani namba moja kwao.

“Malalamiko ya halmashauri za wilaya na miji nchini kuwa na watumishi hewa ni jipu kubwa na lililokomaa. Kama kweli watafanikiwa kupambana na watumishi hao ambao hawapo, mimi nasema nitawapa hongera kubwa,” alisema Damas Makuzi, mkazi wa Mwenge, Dar wakati akifuatilia hotuba fupi ya JPM aliyoitoa juzi, Ikulu ya Dar baada ya wakuu wa mikoa kuapishwa.

RCs (1)Wakuu wapya wa mikoa.

Katika hotuba hiyo, JPM alitolea mfano halmashauri 14 ambapo alisema: “Mwezi Desemba mpaka Januari mwaka huu, halmashauri 14 za mikoa ya Singida na Dodoma kulipatikana kashfa ya malipo hewa ya wafanyakazi 202.
“Ni jambo la aibu kuona kila mwezi serikali imekuwa ikipoteza takribani bilioni 2.5 kutokana na malipo hewa kwa kila mkoa, natoa onyo kwa wakurugenzi wa hazina wa mikoa kuanzia sasa ikigundulika kuna malipo hewa yoyote, basi andika umeumia.”

JPM alisema kuna watumishi walioacha kazi, waliofukuzwa, waliofungwa, walio kwenye likizo bila malipo na waliofariki dunia lakini bado wanalipwa.
Pia, Rais Magufuli aliutumbua jipu mchezo wa ‘pool table’ ambao ni maarufu kwenye baa nyingi nchini. Mchezo huu umekuwa ukichezwa hata muda wa kazi, jambo ambalo rais amewaagiza wakuu hao wa mikoa kuupiga marufuku muda wa kazi kwa vile unachangia watu kutofanya kazi

1 Comment
  1. Nsolo S. Stephen says

    MISHAHARA HEWA KISHAPU:
    Wakati Rais akitoa agizo hili, Wilayani Kishapu wapo wastaafu ambao wameendelea kufaidi malipo ya mishahara kwa zaidi ya miezi 30 hadi Februari 2016. Mifano ni katika Idara ya Elimu Kishapu, kuna Walimu wamestaafu kazi kati ya mwaka 2013 na 2014 ambao wanaendelea kulipwa mishahara. Walimu hao sasa wanapokea malipo ya aina tatu; Pensheni ya kila mwezi, malipo ya nyongeza ya pensheni ya miezi sita_sita na mshahara wa Mwalimu kazini kila mwezi.
    KUNA TUNDU LINAVUJA KATIKA USIMAMIZI WA KAZI.

Leave A Reply