The House of Favourite Newspapers

Mtoto Wa Amina Chifupa Afunguka Maisha Yake Baada Ya Babu Yake Kufariki

0
Mtoto wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), marehemu Amina Chifupa, Abdulrahman Mohammed Mpakanjia.

Stori: Boniphace Ngumije na Gladness Mallya | Risasi Mchanganyiko | Habari

KIJANA Abdulrahman Mohammed Mpakanjia, mtoto wa aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), marehemu Amina Chifupa, kumpoteza babu yake, mzee Hamis Chifupa aliyefariki dunia wiki chache zilizopita, ameelezea maisha yake kwa sasa baada ya kufariki kwa babu yake aliyekuwa akimlea.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Abdulrahman maarufu kama Rahmanino, alisema tangu kufariki kwa mama yake mwaka 2006, ofisi ya taasisi yake, Amina Foundation iliyopo Ustawi- Mwenge ilibaki mikononi mwa babu yake na kwa sasa imefungwa.

“Baada ya babu kufariki ofisi imefungwa na mpaka sasa sijafahamu nani atakayeiendesha. Ninachofanya ni kusubiri kuona ndugu watasema nini maana kwa upande wangu bado ni mdogo na sifikiri kama ndugu wanaweza kukubali kunipa niiendeshe,” alisema Abdulrahman, mwenye umri wa miaka 16, anasoma kidato cha tatu.

Kuhusu mipango ya baba yake kukarabati kaburi la mama yake lililopo mkoani Iringa aliyokuwanayo kabla ya kifo chake, alisema ilikamilika na ameliacha likiwa katika mazingira mazuri.Abdulrahman Mpakanjia akishiriki mazishi ya babu yake.

“Kabla ya babu kufariki alikuwa na mipango ya kwenda kukarabati kaburi la mama kule Iringa. Alifanya hivyo, ameondoka ameliacha likiwa katika mazingira mazuri,” alisema.

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), marehemu Amina Chifupa.

“Kuhusu kukabidhiwa mali za mama bado, hilo halijafanyika kwa sababu ya umri wangu na zitaendelea kusimamiwa na mama zangu wadogo mpaka pale nitakapofikisha umri stahiki.

“Hata hivyo, kikubwa kwa sasa nahitaji kuelekeza nguvu zangu zote kwenye masomo, sihitaji kabisa kufikiria yaliyotokea,” alisema.

Leave A Reply