The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Gadaffi Aenguliwa Kinyang’anyiro cha Urais Libya

0

MTOTO wa kiume wa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi aitwaye Saif al-Islam Gaddafi ameenguliwa katika kinyang’anyiro cha kuwania urais wa nchi hiyo ambapo uchaguzi utafanyika Desemba 24, 2021.

 

Tume ya uchaguzi ilikataa maombi kadhaa ya kugombea kiti hicho yakiwemo ya Saif Gaddafi, ikitaja kuwa sababu ni za kisheria.

 

Gaddafi aliibua utata baada ya kutangaza kwamba atagombea urais wa nchi hiyo huku mahakama ya kimataifa ya uhalifu ikimsaka kwa madai ya uhalifu wa kivita na mauaji wakati baba yake alipokuwa kiongozi wa taifa hilo la Kaskazini mwa Afrika.

 

Maombi ya kuwania urais ya mwanasiasa mwenye ushawishi Khalfa Haftar pia yalisababisha wasiwasi katika nchi hiyo, kwani anakabiliwa na mashitaka katika Mahakama za Marekani, lakini haijawa wazi iwapo yuko miongoni mwa wale ambao wamekataliwa.

 

Waendesha mashitaka wa kijeshi wa Libya walikuwa wameiomba tume ya uchaguzi kuzuia mchakato wa makaratasi ya kugombea ya Gaddafi na Haftar hadi watakapojibu maswali juu ya shutuma dhidi yao.

 

Watu 60 waliwasilisha maombi ya kugombea urais wa Libya kufikia Jumatatu. Mwanaharakati wa haki za wanawake Leila Ben Khalifa, 46, ni mwanamke pekee anayegombe kiti hicho.

Leave A Reply