The House of Favourite Newspapers

Mtoto Wa Lowassa Afichua Siri Nzito – ”Bila Rais Samia Baba Asingefika Hata Jana” – Video

0

MBUNGE wa Jimbo la Monduli, ambaye ni mtoto wa Edward Lowassa, Fredrick Lowassa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupigania afya ya baba yake kabla ya kufikwa na umauti.

“Niseme ukweli kama isingekuwa mama Samia Suluhu Hassan baba yetu asingefika hata hiyo juzi, mama Samia amekuwa ni ndugu, mama mzazi, mlezi wetu kwa kweli hatuna cha kumlipa.” Amesema Lowassa.

Lowassa amesema siku ambayo Rais Samia alikwenda Italia kwenye ziara ya kikazi, hali ya baba yake ilibadilika, hivyo alimtuma mkuu wa majeshi kusimamia matibabu ya baba yake.

“Msiba huu sio wa ukoo wa Lowassa tu bali watoto wanaosoma shule za kata wanaomboleza, Wananchi wanaokunywa maji kutoka ziwa Victoria wanaomboleza, Wanafunzi wanaosoma Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) wanaomboleza na Wananchi wengine wengi wanaomboleza”. Fred Lowassa, Mtoto wa Hayati Edward Lowassa

Leave A Reply