The House of Favourite Newspapers

Maneno Mazito Ya Mstaafu Kikwete, Mzee Warioba Mwili wa Lowassa Ukiagwa – Video

0

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema Hayati Edward Lowassa ameacha alama katika taifa Tanzania ambayo itakumbukwa daima.

Akitoa salamu za rambirambi katika hafla ya kuaga mwili wa Lowassa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Dk. Kikwete ametoa pole kwa Regina Lowassa na kusema Lowassa ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi.

Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema miongoni mwa mambo yaliyowahi kumuumiza marehemu Edward Lowassa, ni pamoja na tukio la jina lake kukatwa ndani ya chama alipojaribu kugombea urais mwaka 1995, huku ikielezwakwamba Hayati Julius Nyerere ndiye aliyepigilia msumari suala hilo.

“Namfahamu Edward tangu akiwa kwenye chama kwa nafasi mbalimbali, baadae akaingia Serikalini wakati sisi tumestaafu. Jambo kubwa Edward alikuwa na imani ya kulitumikia Taifa pamoja na changamoto nyingi alizopitia katika siasa”.Jaji Mstaafu Joseph Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu

Leave A Reply