The House of Favourite Newspapers

MTOTO WA PAPII, UTATA WAIBUKA!

DAR ES SALAAM: Wabongo sio watu wazuri kabisa! Siku chache baada ya msanii wa Muziki wa Dansi, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kutangaza kupata mtoto, Wabongo si wameibuka bwana na kudai eti si wake! Risasi Jumamosi linakuletea ubuyu kamili.  

 

Baada ya kukianika sura kichanga chake hicho Oktoba 28, mwaka huu katika ukurasa wake wa Instagram kama ishara ya kumshukuru Mungu, maoni ya ‘wataalamu’ wa mambo yalitiririka kama matone ya mvua kupinga.

 

Wapo waliojifanya wanajua kukokotoa mahesabu kwa kumhesabia siku alizotoka jela na kulinganisha na muda wa kubeba mimba kisha kujipa majibu kuwa mtoto huyo si wake kwamba huenda amebambikiwa, lakini wapo waliompongeza na kutaka kumjua mwanamke aliyezaa naye.

 

“Duh! Sijaamini ninachokiona, kwa hiyo ulitoka jela siku hiyohiyo na kumpa mtu ujauzito? Si juzijuzi tu umetoka jela? Mara hii mtu kabeba mimba miezi tisa hadi kazaa kweli? Haya bwana kitanda hakizai haramu,” aliandika shabiki wake aliyejitambulisha kwa jina Jasmin.

Mbali na Jasmin, mashabiki mbalimbali walitupia maoni tofautitofauti kuonesha hawaamini kama kweli mtoto ni wa Papii. Kufuatia utata huo, Risasi Jumamosi lilimsaka Papii kwa njia ya simu, alipopatikana alieleza kuwa mtoto huyo ni wake na watu wasiwe na wasiwasi.

 

“Unajua nini? Mimi nilitoka jela Desemba 9, mwaka jana ambapo Desemba 9, mwaka huu (kesho) nitakuwa natimiza mwaka mmoja, na siku niliyotoka nilipokelewa na mama mtoto nikabahatika siku hiyohiyo kumpa ujauzito hivyo naamini mtoto wangu ni wa halali kabisa na niwatoe wasiwasi,” alisema Papii.

 

Papii alipotakiwa kumtambulisha mzazi mwenzake hakutaka kumuweka wazi. Hata hivyo mbali na kichanga hicho, Papii anaye mtoto mwingine aliyezaa na mwanamke aitwaye Mariam.

STORI: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi

DIAMOND ATUA SUMBAWANGA KWA NDEGE, MAPOKEZI YAKE BALAA! (VIDEO)

                  PART 1

 

                 PART 2

Comments are closed.