The House of Favourite Newspapers

MTOTO WA PILI ARUDISHA NDOA YA ESHA BUHET

Esha Buhet

MWIGIZAJI wa filamu Bongo, Esha Buhet amefunguka kuwa mtoto wake wa pili aitwaye Claribel amerudisha ndoa yake iliyokuwa imeshavunjika na kutokuwa na matumaini ya kurudi tena.

Akizungumza na gazeti hili, Esha alisema kila akimuangalia mtoto wake huyo anakuwa na sababu nyingi za kumshukuru Mungu, kwa kuwa ndiye chachu ya kumfanya awepo kwenye ndoa yake mpaka leo.

“Unajua kabla ya ujauzito wa mtoto wangu huyu ndoa yangu ilikuwa haina uhai kabisa yaani ilishikiliwa na uzi mdogo sana, lakini Mungu alipomleta mwanangu huyu na ndoa yangu ikarudi upya kabisa, nashukuru kwa hilo nina maelewano vizuri na mume wangu,” alisema Esha.

 

Comments are closed.