The House of Favourite Newspapers

IGP MSTAAFU AZIKWA DAR – PICHAZ

Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, jana Jumapili, Septemba 30, 2018.

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akitoa heshima baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 

Askari Polisi wakishiriki kushusha mwili wa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu kaburini wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu Mji Mwema Kigamboni ambapo alizikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi-IGP Simon Sirro akiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wastaafu,(kulia) na kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye wakati wa mazishi ya IGP mstaafu marehemu Samwel Pundugu katika makaburi ya Kinondoni.

 

Comments are closed.