The House of Favourite Newspapers

MTOTO WA ROSE MUHANDO AKABIDHIWA TUZO TATU ZA GOSPEL

Amani akiimba mbele ya wageni waalikwa.

Mtoto wa muimbaji nyimbo za Injili, Rose Muhando, Annoint Amani,  jana amekabidhiwa tuzo tatu baada ya kufanya vyema kwenye muziki wa injili. Amani alipewa tuzo hizo na wawakilishi kutoka nchi ya Kenya, Uganda na Kongo DR.

Amani   amepewa tuzo hizo na Kituo cha Redio Aunthetic cha nchini Rwanda katika hafla maalum iliyofanyika nyumbani kwake Mpiji-Magohe jijini Dar. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Kenya, Rwanda na Congo DR. Tuzo hizo ni kwa ajili ya mwimbaji mwenye vionjo vya kipekee, mwimbaji jasiri na mwimbaji wa tofauti.

Matukio katika picha:

Akiwa na waliomkabidhi tuzo.
Akiwekewa mikono na watumishi wa Mungu baada ya kupewa tuzo hizo.
Mwakilishi kutoka Redio Authentic ya Rwanda, Issa Kalinijabo, akieleza sifa zilimfanya Amani atwae tuzo hizo.
Wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri.
Akiwa na tuzo zake.

HABARI: ZAINA MALOGO / GPL PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

 

 

Comments are closed.