The House of Favourite Newspapers

Mwanzilishi wa Bendi za Backstreet Boys na NSYnc Afariki Dunia

0

Lou PearlmanMwanzilishi na Kiongozi Mkuu wa bendi za Boy Bands ambazo ni  Backstreet Boys na pamoja na ile ya NSYnc, Lou Pearlman amefariki Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 62 katika Kitongoji cha Miami nchini Marekani.

Pearlman alikuwa amefungwa gerezani kwa kosa la udanganyifu wa mpango wa Ponzi uliogharimu dola milioni 300. Ilidaiwa kuwa alidanganya familia, marafiki, wawekezaji na benki kwa kuwashawishi kuwekeza fedha zao kwenye kampuni bandia kwa takriban miaka 20, kosa ambalo lilipelekea akamatwe na afungwe jela mwaka 2008.

23xp-pearlman-master675Justin Long, ambaye ni msemaji wa Kitengo cha Kuzika wafungwa huko Miami alisema, bwana Pearlman amefariki akiwa hospitali alikokuwa akitibiwa tatizo la moyo kushindwa kusukuma damu ipasavyo (Cardiac Arrest).

Mwambaji wa NSYnc Lance Bass alituma ujumbe katika Twitter akisema kuwa Pearlman hakuwa mfanyibiashara mzuri lakini hangekuwa pale alipo bila ushawishi wake.

lou-pearlman-mad-about-the-boys-01

“Habari ni kwamba #LouPearlman amefariki.Hakuwa mfanyibiashara mzuri, lakini sidhani nisingekuwa nikifanya kitu ninachokipenda sana bila ushahwishi wake. Pumzika kwa amani Lou”.

23pearlman-obit-master768

‘Ulafi ulimtawala’.

Pearlman alivutiwa na ufanisi wa bendi ya New Kid on The Block na kuanzisha kampuni yake ya kurekodi ambapo alizindua bendi ya vijana wenye vipawa kwa Jina Backstreet Boys.

Bendi hiyo iliuza vibao milioni 130. NSync pia walifanikiwa pakubwa na kuweza kuuza vibao milioni 55.

Pearlman baadaye aliongoza bendi nyingine za vijana kama vile LFO, Take 5, Natural na O-Town, na kundi la wasichana, lililoshiriki katika wimbo wa mwanamuziki Britney Spears.

Leave A Reply