The House of Favourite Newspapers

Mugalu Out Simba, Ajitonesha Nyonga

0

MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Mkongomani, Chris Mugalu, jana ameukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara baada ya kujitonesha maumivu ya nyonga akiwa kambini Sumbawanga.

 

Mugalu anakuwa janga jingine katika safu ya ushambuliaji ya Simba ambayo tayari ina majeruhi wengine ambao ni Meddie Kagere na John Bocco.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, Mugalu alijitonesha maumivu hayo katika mazoezi ya mwisho ya juzi Jumatano.

Mtoa taarifa wetu alisema kuwa mshambuliaji huyo alianza kupata maumivu hayo kwenye mchezo wa kirafiki waliocheza dhidi ya Mlandege FC ya Zanzibar kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar wiki iliyopita.

 

Alipotafutwa Daktari Mkuu wa Yanga, Yassin Gembe kuzungumzia hilo, simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa, pia alitafutwa Meneja Mkuu, Patrick Rweyemamu kuzungumzia hilo naye simu yake ilikuwa haipatikani.

Stori: Wilbert Molandi na Ibrahim Mussa

“SIMBA Wangepigwa TANO, Hawana KIKOSI Kipana, CHAMA Ana MCHANGO WAKE” – MWL KASHASHA…

Leave A Reply