The House of Favourite Newspapers

Muhimbili Kufunga Mitambo ya Kitabibu Katika Hospitali Tatu za Mikoani

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) iliyopo jijini Dar es Salaam, ipo katika harakati za kufunga mitambo ya ‘Telemedicine’ katika mikoa mitatu ikiunganisha hospitali saba ambazo ni Morogoro Mjini, Tuliani, Kilosa, Lindi Mjini, Nyangao na Nachingwea ambao watawasiliana moja Kwa moja na Hospitali ya Taifa Muhimbili katika utoaji huduma zake wakati mgojwa akipatiwa matibabu.

Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Hedwiga Swai (katikati) akizungumza jambo. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Julieth Magandi pamoja na Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, John Stephen.

Hayo yamesemwa leo Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Muhimbili, Dkt. Hedwiga Swai wakati aakielezea mipango mbalimbali na utekelezezaji wake katika hospitali hiyo.

Aidha, Dkt. Swai amesema kuwa matibabu ya wagonjwa wa dharura (EMD) wameongezeka kutoka wagonjwa 100 hadi 150 Kwa siku hapo awali na kufikia wagonjwa 200 hadi 300 hivi sasa.

Akielezea kuhusu huduma ya matibabu figo na kuchuja damu, amesema hiyo inapanua huduma ya kuchuja figo kutoka vitanda 17 vilivyopo sasa na kufikia vitanda 42 ambavyo vinategemewa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu 2017.

PICHA NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.