The House of Favourite Newspapers

Muigizaji na Muongozaji wa Filamu G Marimuthu Afariki

0

Tasnia ya Filamu nchini India inaomboleza kifo cha Muigizaji na Muongozaji maarufu wa Filamu G Marimuthu, aliyefariki dunia Septemba 8, 2023 kwa mshtuko wa moyo.

Marimuthu aliyekuwa akifanya kazi na tasnia hiyo kwa upande wa lugha ya Tamil, alianguka akiwa katika studio ya televisheni huko Chennai na alitangazwa kuwa amefariki baada tu ya kufikishwa hospitali.

Muigizaji huyo mkongwe ameigiza zaidi ya filamu 50 na hadi mauti yanamkuta alikuwa akirekodi kazi ya tamthilia ya Ethirneechal (Swimming Against The Tide)ambamo alikuwa mmoja wa waigizaji wakuu.

Moja ya Filamu zake za mwisho kuigiza ni “Jailer” ambayo ni ya tatu kwa mafanikio katika Filamu za India kwa mwaka huu.

#EXCLUSIVE: LULU AVUNJA UKIMYA – “NIMETUA MZIGO wa MAMA KANUMBA, NITAUBEBA MSALABA HADI KUFA”…

Leave A Reply