The House of Favourite Newspapers

MultiChoice, KCB Waungana Kusherekea Wiki Ya Huduma Kwa Wateja!

0
Timu ya mpira wa miguu ya MultiChoice Tanzania na KCB Bank katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mtanange wa kukata na shoka baina yao.

Kampuni ya MultiChoice Tanzania kwa kushirikiana na benki ya KCB  Oktoba 10, 2020 wameungana kuendeleza shamra shamra za wiki ya huduma kwa wateja kwa kufanya matembezi maalum, mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu pamoja na michezo mbalimbali  mapema leo jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza katika viwanja vya Gymkhana Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja MultiChoice Tanzania, Bi. Ngwitika Mwakahesya alisema kuwa “Wiki hii huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, lakini kwetu MultiChoice kila siku tunazingatia swala muhimu la kutoa huduma kwa wateja wetu wote kwa viwango vinavyotakiwa.

Mpambano kati ya timu ya MultiChoice Tanzania (DSTV) na KCB Bank katika mchezo wao maalum wa ‘Wiki ya Huduma kwa wateja’ uliofanyika kwenye uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam mapema jana Oktoba 10, 2020.

“Mwaka huu MultiChoice tumeipa wiki hii kauli mbiuExceeding Customers Expectationstukimaanisha kuendelea kuwajengea wateja wetu imani katika huduma kwa kuwapatia huduma zenye ubora wa hali juu.

 

Katika mwezi huu pia MultiChoice tumetambua umuhimu wa wadau mbalimbali ambao tunashirikiana nao katika shughuli za kila siku za kibiashara hivyo tumezingatia hilo na ndiyo maana leo tuko hapa na wenzetu wa Benki ya KCB kwa ajili ya kushiriki michezo mbalimbali hususani  mbio za kilometa 5 na mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu iliyomalizika kwa sare ya goli 1-1 .

Wafanyakazi wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania katika picha ya pamoja mapema Oktoba 10, 2020 katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Mbali na shamra shamra hizi pia, napenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha wateja wetu juu ya huduma zetu mbadala ambazo zimelenga kuleta ufanisi na kuwapatia urahisi endapo watakua wanahitaji huduma kwa haraka ikiwemo kuangalia salio, kulipia kifurushi na kubadlisha aina ya kifurushi anachotumia.

 

Wateja wetu wanaweza kupata huduma hizo kwa njia ya WhatsApp kupitia namba 0677 666111, kwa njia ya USSD kwa kubonyeza *150*53#, kwa wateja wetu wenye simu za kidigitali wanaweza kuapata huduma zetu pia kwa kupakua App ya MyDStv. Hivyo mteja wetu anaweza kupata huduma akiwa nyumbani kwake kwa haraka Zaidi.

 

Alimaliza kwa kueleza kuwa mteja wa DStv pia anaweza kuendelea kufurahia huduma mbalimbali zinazopatikana katika kifurushi alichokifanyia malipo kupitia huduma ya DStv Now mahali popote kupitia simu yake ya mkononi, Laptop pamoja na Tablet mbali na huduma anayoifurahia kupitia televisheni yake awapo nyumbani.

Leave A Reply