The House of Favourite Newspapers

Multichoice Tanzania kufadhili ndoa ya Wapendanao

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande, akielezea namna mchakato wa kuwapata washindi hao ulivyoendeshwa.

 

KAMPUNI ya Multichoice Tanzania, kupitia kipindi chake cha Maisha Magic Bongo, kinachorushwa katika king’amuzi chao cha DSTV, Chanel namba 160, imeamua kutumia siku ya leo ya Wapendanao kuwatangaza washindi wa shindano la Harusi ya Ndoto Yako, Solomon Mwaigwisa na mchumba wake Magreth Richard, baada ya kuibuka washindi kwenye shindano hilo na kutoa zawadi ya kuwaandalia shughuli nzima ya ndoa yao inayotarajiwa kufungwa Aprili mwaka huu.

 

Zawadi ya king’amzi ikikabidhiwa kwa Eva Sindika (katikati) baada ya kuibuka mshindi kwenye moja ya droo ndogo iliyochezeshwa kwa ajili ya wanahabari waliohudhuria shughuli hiyo kwenye makao makuu ya multichoice Tanzani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza katika utambulisho huo Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande, Channel ya Maisha magic Bongo imeamua kuwatunuku watazamaji wake zawadi hiyo kwa mujibu wa kipindi hicho ambacho huonyesha matukio mbalimbali ya Harusi.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande, akijibu moja ya swali lililoulizwa na waandishi kwenye hafla hiyo.

 

“Kipndi chetu cha Harusi yetu tulikianzisha tangu mwak 2017,ambapo kimekuwa kikirusha mambo mbalimbali ya harusi huku kikiangazia zaidi maisha ya wanandoa walikotokea hadi kufikia hatua hiyo muhimu ya kufunga ndoa.

 

“Tangu ilipoanza Maisha Magic Bongo, iliamua kuanzisha shindano la Harusi ya ndoto yako, ambapo weasjiriki walitakiwa kujibu maswali mbalimbali yahusianayo na na kipindi cha Harusi Yetu.

 

Baadhi ya wanahabari wakichukua matukio yaliyokuwa yakiendelea mahali hapo.

 

“Shindano hilo lilikuwa na msisimko mkubwa sana kiasi cha kufikisha washirikia 1,112 na kuingia kwnye mchujo ambapo kati yao walisalia 448 na wao wakachujwa hadi tulipopata washindi hawa wawili na kuamua kwa pamoja kuwagharimia kila kitu katika harusi yao.

 

“Mbali na kuwafanyia harusi yao pia tutawagharimia shughuli ya kufanya fungate avbapo tutawasafirisha kwa gharama zetu hadi Mombasa nchini Kenya katika Hoteli ya kitalii ya Voyager Beach,” alisema Maharage.

Na Musa Mateja | Global Publishers

Comments are closed.