The House of Favourite Newspapers

Mume Aliyemfunga Mkewe Mtini Kortini

0

Ampiga mkwara mwandishi wa Uwazi

Stori: Gregory Nyankaira,  UWAZI

MARA: Mwanamke mmoja Jeni Marwa,  (pichani)  mkazi wa Kijiji cha Singu, Kata ya Kukirango, Wilaya ya Butiama mkoani Mara aliyefanyiwa kitendo cha udhalilishaji na mumewe, Nyango Hakimu, kwa kumfunga kamba mtini na kumpa kichapo kikali kwa madai ya kutopata ujauzito tangu amuoe miaka saba iliyopita na habari zake kuandikwa katika gazeti hili toleo lililopita, amemfikisha Mahakama ya Mwanzo ya Kukirango mumewe akidai ampe talaka.

Mwanamke huyo ametinga katika mahakama hiyo Februari 18, mwaka huu mbele ya Hakimu Erick Kimaro baada ya shauri kuhamishwa kutoka Baraza la Usuluhishi la Kukirango ambako awali lilifunguliwa.

Akiwa mahakamani hapo Jeni alisema: ” Ni heri nipewe talaka ili nimtafutie mwanaume huyu mahari yake kuliko kung’ang’ania ndoa ambayo imegeuka kuwa jenahamu, anaweza kuniua kwa kichapo.”

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa wakati wowote wiki hii na mwanamke huyo ameiomba serikali kumpa msaada wa kisheria kwa vile yeye amefungua kesi ya kudai talaka tu. Kwa sasa anaishi kwa wazazi wake katika Kijiji cha Mwanza Buriga, Butiama, Mara.

     Aidha, katika hatua nyingine mwandishi wa habari hizi anaishi katika wakati mgumu baada ya kufuatwa nyumbani na mume wa mwanamke huyo kwa madai kuwa amefichua siri na kumtishia kumkomesha kwa gharama yoyote ile.

 “Mwanamke huyo ni halali yangu nina uwezo wa kumfanyia lolote lile maana wazazi wake wana mali yangu, kwa nini mimi niishi na mwanamke ambaye hazai, kumpiga tu umetoa habari, yanakuhusu nini wewe na hizo picha ulizipataje kama si umbeya?” alifoka mume huyo.

Leave A Reply