The House of Favourite Newspapers

MUNA, BABA PATRICK VITA MPYA

Rose Alphonce Nungu ‘Muna Love’,

DAR ES SALAAM: Baada ya sarakasi za hapa na pale kisha ukimya kutawala, hatimaye mwigizaji wa filamu za Kibongo, Rose Alphonce Nungu ‘Muna Love’, ameibua vita mpya na mumewe wa ndoa, Peter Zakaria Komu ‘Baba Patrick’ kufuatia kutinga mahakamani kudai talaka na nyumba waliyokuwa wakiishi iliyopo Mwananyamala-Kisiwani jijini Dar.

 

Chanzo cha habari cha Gazeti la Ijumaa kilitonya kuwa Muna alikwenda mahakamani ili kudai talaka yake na kugawana vitu ambavyo walichuma pamoja walipokuwa wote.

 

“Unajua ninamshangaa sana Muna, amekwenda mahakamani, anasema ile nyumba ni ya kwake, lakini wauzaji wa kile kiwanja wapo na kama haitoshi hadi mafundi waliojenga wapo kwa hiyo tuiachie mahakama ifanye kazi yake.“Talaka sawa, kama yeye ameamua, siyo mbaya kwa kuwa hawapo pamoja kwa kipindi kirefu. Kwa hiyo kama anadai talaka ni sawa tu, kwa kuwa tunasikia anahitaji kuwa huru na pengine anataka kuolewa na mwanaume mwingine.Image result for MUNA NA Peter Zakaria

“Lakini kuhusu nyumba, walijenga wakiwa mume na mke, nafikiri mahakama itafanya kazi yake,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa Muna na Baba Patrick. Baada ya kusikia ishu hiyo, Gazeti la Ijumaa lilimtafuta Muna bila mafanikio, lakini lilimpata Peter (Baba Patrick) ambaye alikuwa na haya ya kusema juu ya sakata hilo;

 

“Ni kweli nilikwenda mahakamani Magomeni (Dar) na Muna. Anataka mgawano wa mali na talaka. Ninachojua talaka zina process (taratibu) zake, lakini kesi ni tarehe 20 ya mwezi ujao (Februari) hivyo Muna anatakiwa afike na mashahidi. Muna na Peter waliingia kwenye mgogoro tangu walipofiwa na mtoto wao, Patrick ambapo kuliibuka mkanganyiko na sintofahamu ya kujua baba halisi wa mtoto kufuatia uwepo wa baba mwingine, Casto Dickson.

 

Waandishi: Neema Adrian na Imelda Mtema,

Stori: WAANDISHI WETU, IJUMAA

Comments are closed.