The House of Favourite Newspapers

Msukuma: Miradi ya Mabilioni ya Pesa, Haina Impact kwa Taifa – Video

0

MBUNGE  wa Geita kupitia CCM, Joseph Kasheku maarufu kama Msukuma, ameshauri mabilioniya fedha  yanayowekezwa na serikali kwenye miradi ambayo haizalishi, kuwekezwa kwa watu wa hali ya chini.

 

Amesema: “Nitoe tu ushauri kwa serikali, katika kipindi kilichopita,  serikali imekuwa na miradi mikubwa ya mabilioni ya pesa ambayo haina impact yoyote kwenye taifa, Watanzania wa chini hatuoni faida ya miradi mikubwa ambayo serikali imewekeza mabilioni ya pesa.

 

“Tuna Soko la Morogoro, Machinga Complex na sasa la Ndugai, wote ni mashahidi yamefeli, ni mabilioni mangapi yametumika? Kwa sababu wasomi mnashindwa kutafakari kwamba mnapojenga masoko au mastendi makubwa ya mabilioni ile ni huduma na nyinyi mnaweka kama vitegauchumi.

 

 

“Masoko na mastendi makubwa yanageuzwa vitegauchumi badala ya kuwa huduma, maskini hawawezi kwenda, hili Jengo la Bunge lilitumia hela nyingi za Watanzania na sisi tungekuwa tunalipia pesa getini ili kuingia humu, tungeona uchungu yale tunayowapangia wananchi kule chini.

 

 

“Nilivyoanza ubunge nilikuwa Kamati ya Ardhi, tulienda kukagua mradi Morocco nyumba za maskini, tuligombana sijui ndiyo maana spika ukanihamisha kunipeleka madini, niliwaambia uchumi ukiyumba humu tutalaza popo, leo jengo limeisha hakuna kinachoendelea.

 

 

“Naipongeza sekta ya madini kwa kuongeza kipato kutokana na kupokea mawazo ya wadau wa madini, nampongeza rais kwa kutupa nafasi sisi wa darasa la saba tukaishauri serikali na akatusikiliza, leo serikali inavuna mabilioni kutokana na mawazo yetu darasa la saba.

 

 

“Haya mambo ambayo tunaona rais ameyafanya tunaweza kuona namna tukamwongezea muda, kwani kitu gani mbona wenzetu wamefanya? Ina maana sisi Watanzania tunaijua demokrasia zaidi ya Wachina ambao ni matrilionea? Wamefika mahala wakaona tumuongeze mtu hata miaka ishirini mbele,” amesema Msukuma.

 

 

Leave A Reply