The House of Favourite Newspapers

Mutungi Ataka Vyama Vimalize Migogoro

0

1.Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (wa pili kushoto) akizungumza na wanahabari.

MSAJILI wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi,  amevitaka vyama vya siasa nchini vyenye mpango wa kufanya maandamano au mikutano ya kuhamasisha wanachama wake viache mara moja ili kutafuta suluhu za changamoto zinazowakabili kupitia majadiliano ya pamoja.

2.Kutoka kushoto ni Msajili Msaidizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,  Sisty Nyahoza, Jaji Francis Mutungi na Mkurugenzi wa Kamati ya Fedha ya Baraza la Vyama Vya Siasa, Constantine Akitanda.

Jaji Mutungi ameyasema hayo leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wanahabari ambapo amesema migogoro na changamoto za kisiasa zinazovikabili vyama vya siasa visipojadiliwa katika meza moja vinaweza kusababisha kuvunjika kwa amani ambayo imejengwa kwa muda mrefu na waasisi wa taifa hili.

3.Wanahabari wakichukua tukio hilo.

Mutungi amesema akiwa mlezi wa vyama vya siasa na katibu wa vyama hivyo, amevitaka vyama vya siasa kutumia mkutano maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa unaotarajiwa kufanyika Agosti 29,30 mwaka huu kujadili changamoto zinazowakabili kwa njia ya amani na maridhiano badala ya kufanya maandamano ambayo yanaweza kuhatarisha amani nchini.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply